USARIFU WA TAKA NA KUTENGEZA BIDHAA MBALIMBALI.

 

Waziri wa ardhi, nishati maji  na mazingira mhe salama aboud talib amesema elimu zaidi inahitajika kwa wananchi kujua umuhimu wa usarifu wa taka na kutengeza bidhaa mbalimbali.

Akifungua semina ya wadau wa nchi za  afrika wa kujadili namna ya kukubaliana na usarifu wa taka taka hapa zanzibar amesema mradi wa usarifu wa taka ni muhimu kwani wananchi wateweza kutambua namna ya kuzitunza taka kavu na taka za maji maji.

Amesema kituo cha sayansi na mazingira cha india kwa ushirikiano na mamlaka ya usimamizi wa mazingira zimetiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa mradi huo kwa miaka mitatu ili zanzibar iweze kukua kichumi zaidi kupitia taka zinazozalishwa .

Mkurugenzi mkuu mamlaka ya usimamizi wa mazingira sheha mjaja amewataka wanachi kutambua kwamba takataka si uchafu bali wanaweza kuzisarifu na kufanya bidhaa.
Mkurugenzi wa kituo hicho shandra bhurshan amesema nchi nyingi duniani zimekuwa katika mfumo wa kusarifu takan na kujiongezea kipato kupitia takataka.

Wakati huo huo uzinduzi wa usarifu wa takataka umeafanyika katika shehia ya shauri moyo kwa majaribio ambaop wananchi mia mbili wamepatiwa vifaa vya kusarifu takataka. Mwisho.