USHAJIHISHWAJI WA SUALA LA UGATUZI WA MADARAKA

 

Ushajihishwaji wa  suala  la  ugatuzi  wa  madaraka  kufikia  ngazi  ya  shehia   utaleta  mwamko  kwa  jamii  dhidi  ya  uibuaji  wa  miradi  iliyopewa  kipaumbele  katika  utekelezaji  wake  ndani  ya  shehia  husika.

Wakitoa  michango  yao  washiriki  wa  mafunzo  elekezi   juu  ya  kupanga  mipango    na  ushirikishwaji wa  wananchi   juu  ya  harakati   za  kimaendeleo   katika  shehia   yaliotolewa  na  chama  cha  malezi  bora  tanzania  umati   wamesema hali  hiyo  itasaidia    usikilizwaji  wa  maoni  yao  katika  miradi  inayozihusu  shehia  ili  iweze  kukamilika  kwa  wakati.

Wamesema  jamii  ikipatiwa  elimu  hiyo  ya  ugatuzi   ipasavyo  itaondoa  vikwazo vingi  katia  shehia  ikiwemo  ya  watendaji   kuachana  na  itikadi  za  kisiasa    dhidi  ya utekelezaji wa   miradi  ambayo  mara  nyingi  haitekelezeki.

Akitoa  tamko  la  ufungaji  wa  mafunzo  hayo    mkuu  wa  kikosi  kazi  cha   jumuiya  ya umati  bi  hidaya  hassan  amesema   umefika  wakati  kwa  wakaazi  wa  kila  shehia  kuzitumia  fursa  zilizopo  ili  kuweza  kupiga  hatua   za  haraka  kimaendeleo  ndani  ya  shehia  .