USHIRIKI MZURI KATIKA HARAKATI ZA MAANDALIZI YA IJITIMAI YA KIMATAIFA

 

 

waumini wa dini ya kiislam wamepongezwa kwa ushiriki mzuri katika harakati za maandalizi ya ijitimai ya kimataifa inayotarajiwa kufanyika mei 19 kidoti mkoa wa kaskazini unguja.

Akizungumza katika eneo hilo amir sayfulhaq kutoka uganda amesema ni jambo jema kuona waumini wa zanzibar  wanashirikiana katika mambo ya kheri ambayo yatawapatia fadhila.

Amefahamisha kuwa zanzibar ni nchi ya kuigwa kwani wananchi wake wamekuwa na uvumilivu katika kusimamia masuala ya dini na kuomba ushirikiano huo uendelezwe.

Wakielezea maandalizi ya ijitimai hiyo wajumbe wa kamati wamesema  wamejipanga vizuri na kuhakikisha wageni wataofika katika ijitimai hiyo wanakuwa katika mazingira mazuri na kupata huduma zilizo bora.

Wamewaomba waislam kuendelea kutoa michango ikiwemo vifaa vya matumizi vikiwemo vikombe, mabusati na vyakula  ili viweze kusaidia wageni watakaohudhuria .