USHIRIKIANO MDOGO WA JAMII KATIKA KUPINGA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

 

Ushirikiano mdogo wa jamii katika kupinga vitendo vya udhalilishaji na tamaa kwa wazazi kuwageuza watoto kuwa kitega uchumi vyao ni miongoni mwa changamoto zinazosababisha kuongezeka vitendo vya ubaguzi,udhalilishaji na ukatili dhidi  ya watoto katika mkoa wa kaskazini unguja.

Akisoma risala ya watoto wa mkoa huo katika maazimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyoandaliwa na mtandao wa walimu wanaosimamia vilabu vya  watoto vya kupinga udhalilishaji mkoa wa kaskazini unguja, mtoto  amina machano ali amesema baadhi ya wanajamii hawatoi ushirikiano kwa wanaharakati wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwa watoto pindi wanapohitajika katika kutoa ushahidi mahakamani pamoja na wazazi kuwaoza watoto wakiwa katika umri mdogo.

Amesema  jambo kwa kiasi kikubwa  linasababisha kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto mkoani humo.

Nae mratib wa shirika la action aid kanda ya unguja bi khadija ali juma amesema watoto wengi wanapatwa na majanga ya udhalilishaji kutokana na kukosa kujitambua hivyo shirika  limeamua kupambana  kutokomeza vitendo hivyo kwa kuanzisha club za watoto ili kuwajengea uwelewa wa kutambua haki zao.

Mkuu wa wilaya ya kaskazini “b” rajab ali rajab amewataka masheha wa wilaya ya kaskazini “b” kutoshiriki katika upatanishaji wa kesi za udhalilishaji ili kukomesha vitendo hivyo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja mhe: vuai mwinyi mohamed amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao ili wapate kuwafunza, kuwauliza na kuwapa nafasi ya kujieleza ili waweze kusema mambo yanayo wasibu na sio kuwalaumu pindi wanapokwenda kinyume na maadili.

Chimbumbuko la siku ya mtoto wa afrika ni mauaji ya watoto mia sita katika kijiji cha soweto nchini afrika ya kusini mwaka 1976 wakati wa utawala wa kibaguzi nchini humo