USHIRIKIANO WA SEKTA BINAFSI UMESAIDIA UTAFITI ULIOFANYWA NA MTAALAMU MWELEKEZI

Waziri wa kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto mh. Moudeline castico amesema ushirikiano wa sekta binafsi umesaidia utafiti uliofanywa na mtaalamu mwelekezi kuhusu kima cha chini cha mshahara kwa sekta hiyo.
Akizungumza na uongozi wa africa house na perfrct coffee, akiwa na kamishna wa kazi bi fatma iddi na naibu katibu mkuu wa wizara hiyo bi maua makame amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kujenga mazingira ya wafanyakazi kwa matumaini ya baadae.
Mh. Castico amesema wizara haikutaka kufanya njia ya mkato katik akupanga mishahara kwa sekta binafsi bali imeamua kumtumia mshauri mwelekezi ili kuona hali ya mishahara ilivyo kwa sekta hiyo.
Amewasisitiza waajiri kuwajengea mazingira mazuri wafanyakazi wao ikiwemo maslahi bora ili kukidhi mahitaji yao.
Afisa mradi rasilimali watu katika hoteli ya africa hosue abdalla shaaban ameishukuru serikali kwa ushirikiano wake na sekta binafsi katika mambo mbalimbali ya maendeleo na wako tayari kupokea maelezo ili kuleta ufanisi kwa pande zote.