USHIRIKIANO WA WAZAZI KATIKA KUWALEA WATOTO KIMAADILI KUTAPUNGUZA VITENDO HATARISHI KWA WATOTO

Ushirikiano wa wazazi katika kuwalea watoto kimaadili kutapunguza vitendo hatarishi kwa watoto ikiwemo kubakwa pamoja na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Hayo yamefahamika huko katika ukumbi wa mikutano gombani wakati wa kikao cha uzinduzi wa mradi wa malezi bora kwa watoto na kupinga udhalilishaji unaosimamiwa na jumuiya ya zapha plus
akifungua mkutano huo katibu tawala wilaya ya chake nd abdalla rashid amesisitiza jamii kuwa na malezi ya pamoja na kufuatilia nyendo zawatoto ili kubaini tatizo na mapema.
Nae mratib wa zapha plus pemba nd abdalla omar amesema suala la udhalilishaji kwa watoto sio kubaka tuu lakini hata kumkosesha mtoto elimu ni udhakilishaji na kunapelekea mtoto kufanya matendo yenye madhara bika kujielewa.
Wakichangia katika mkutano huo washiriki mbali mbali wamesema.
Uzinduzi huo wa mradi wa malezi bora kwa watoto na kupinga uzalilishaji unategemewa kutekelezwa katika shehia 45 za zanzibar ukiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kutokomeza vitendo vya udhalilishaji lakini uzinduzi wake
Ni sehemu ya shughuli zinazoambatana na maadhimisho ya siku ya ukumwi duniani