USIMAMIZI WA SHERIA KATIKA UTENDAJI WA KAZI

Kamishina wa kazi kutoka wizara ya kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto fatma ali amesisitiza usimamizi wa sheria katika utendaji wa kazi ili kuwepusha migogoro.
Akifungua mafunzo kwa wajumbe wa chama cha wafanyakazi wa mawasiliano na usafirishaji zanzibar (cotwu) amesema usimamizi wa sheria utasaidia kuweka nidhamu pamoja na uwajibikaji kati ya waajiri na waajiwa katika sehemu za kazi.
Aidha amewataka wafanyakazi kutodharau vyama vya wafanyakazi ili kupata fursa ya elmu kuhusu sheria za kazi na kutetea haki zao.
Mwenyekiti wa taifa saleh mohammed na katibu mkuu wa chama cha cotwu mohammed ali salum akiwasilish mada ya katiba ya chama cha wafanyakazi amewomba wafanyakazi kuungana pamoja ili kuwa na suti moja katika kudai haki zao