UTAFITI WA KUANGALIA MARADHI YANAYOATHIRI MWANI

Idara ya mazao ya baharini inaendelea na utafiti wa kuangalia maradhi yanayoathiri mwani katika vijiji mbalimbali vya unguja.
Afisa idara hiyo mohammed soud amesema kwa sasa wanshirikiana na mtaalamu kutoka ufilipino ambapo utafiti huo utafinyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza na jumuiya ya wakulima wa mwani zanzibar amesema miongonimwa masuala yanayoangaliwa ni pamoja na ubora na sababu ya mwani kukukumbwa na maradhi yasiyojulikana yanayokwamisha kuota ili kupata ufumbuzi wake.
afisa soud ameongeza kuwa athari hizo hasa kwa maradhi hayo yaliyobainika mwaka 2012 yamesababisha kushuka uzalishaji wa mwani hali iliyowafanya baadhi ya wakulima kuacha kilimo hicho.
Nao wanajumuiya hiyo wametoa maoni yao na wameiomba serikali kuangalia kwa kina matatizo yanayowakabili kwa kushirikiana na kampuni ya uuzaji mwani ili kuweza kutatua matatizo hayo.
Kwa mujibu wa taarifa uzalishaji wa mwan i umeshuka kutoka zaidi tani 16 elfu hadi tani elfu kumi na moja mwaka kati ya mwaka 2015 na 2016 kutokana na maradhi hayo.