UTAPELI WA KUWAUNGIA UMEME KINYUME NA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SHIRIKA.

Wanachi wa mtaa wa Kwarara Madina jimbo la Kijitoupele wameanza kufanyiwa vitendo vya utapeli baada ya mtu mmoja kuwaungia umeme kinyume na utaratibu uliowekwa na shirirka.
mtu huyo anaedaiwa kuwa ni mfanyakazi wa shirika la umeme zeco aliwaungia umeme wananchi hao wakiwa wameshamlipa fedha bila ya kupata huduma takriban miezi minne sasa.
salum abdalla ni afisa uhusiano wa shirika hilo amesema wameamua kuwakatia umeme wananchi hao baada ya kupata taarifa huku wakiendelea kumtafuta mtu huyo anaehusika kufanya wizi huo katika shirika hilo.
kufuatia hali hiyo mkaazi mmoja wa maeneo hayo bibi fatma hija kombo ambae amefikwa na mkasa huo ameiomba serikali kuwatafuta watu wanaofanya vitendo vya hujuma za wizi kwa wananchi pamoja na kuibia serikali.