UTARATIBU WA MADAKTARI WA MISRI KUTOA HUDUMA ZA AFYA UMEANZA KULETA MATUMAINI

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amesema utaratibu wa madaktari wa misri kutoa huduma za afya kwa watanzania umeanza kuleta matumaini kwa watu wengi.
Amesema utaratibu huo unazingatia uhusiano wa kibalozi uliopo baina ya nchi mbili hizo.
Balozi seif ali iddi amesema hayo ofisini kwake vuga mjini zanzibar wakati akibadilishana mawazo ya timu ya madaktari kutoka hospitali ya chuo kikuu cha el –shady kiliopo alexandria nchini misri waliopo zanzibar kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa mbali mbali.
Alisema amesema wakati umefika kwa uongozi wa vyuo vikuu tofauti vya nchini misri kuzingatia uongezaji wa fursa za masomo ya juu kwa wanafunzi wa tanzania hasa katika sekta ya afya na elimu.
balozi seif alifahamisha kwamba hatua hiyo itasaidia kwenda sambamba na uimarishaji wa sera za afya na elimu zilizolenga kuimarisha elimu ya msingi kwa wanafunzi pamoja na huduma ya afya ya msingi hasa vijijini.
Makamu wa pili wa rais wa zanzibar aliueleza ujumbe huo wa madaktari tisa wa hospitali ya chuo kikuu cha el – shady alexandria nchini misri kwamba zanzibar imeweka mkakati wa kuwa na huduma za afya ya msingi kila baada ya kilomita tano.
Mapema kiongozi wa timu ya madaktari hao kutoka hospitali ya chuo kikuu cha el – shady alexandria nchini misri profesa saber waheeb amesema timu yake tayari imeshatoa huduma za afya kwa tariban mara ya nnne sasa.
Profesa waheeb amesema wataalamu wa timu hiyo hutoa huduma za upasuaji kwa watoto walioziba njia ya mkojo, haja kubwa pamoja na uvimbe wa tumbo wakitarajia kuwafanyia huduma za upasuaji wagonjwa wasiopungua 38.
Timu hiyo ya madaktari mabingwa wa hospitali ya chuo kikuu cha el –shady kiliopo alexandria nchini misri wanamalizia kutoka huduma hizo katika hospitali kuu ya mnazi mmoja mjini zanzibar.
Akiiongoza timu hiyo ya madaktari mabingwa wa hospitali ya chuo kikuu cha el –shady kiliopo alexandria naibu waziri wa afya mheshimiwa harous said suleiman amesema ujio wa madaktari hao umeleta faraja kwa wagonjwa mbali mbali ambao wangelazimika kutumia gharama kubwa kupata huduma hizo nje ya nchi.
Naibu waziri harous aliushukuru uongozi wa chuo cha el –shady alexandria nchini misri kupitia hospitali yake kwa uamuzi wake wa kutenga wataalamu wa afya kutoa huduma zanzibar katika mpango endelevu unaofanyika kila kipindi.