UTAWALA WA RAIS WA MAREKANI UMEJIONDOA KUTOKA MAKUBALIANO YA UMOJA WA MATAIFA

Utawala wa rais wa marekani donald trump umejiondoa kutoka makubaliano ya umoja wa mataifa kuhusu namna ya kuimarisha hali za wakimbizi na wahamiaji.
Taarifa ya serikali ya marekani imesema mkataba huo hauendani na sera zake na imemfahamisha katibu mkuu wa umoja wa mataifa, antonio guterres kuwa inasitisha kushiriki katika makubaliano hayo.
mwezi septemba mwaka jana, mkutano mkuu wa umoja wa mataifa wa nchi wanachama 193 ulipitisha kwa kauli moja azimio la kisiasa kuhusu wahamiaji na wakimbizi likiahidi kulinda haki za wakimbizi, kuwasaidia kupata hifadhi na kuhakikisha wanapata elimu na ajira.
Balozi wa marekani katika umoja wa mataifa, nikki haley amesema nchi yake itaendelea na kile alichokitaja ukarimu wake katika kuwasadia wakimbizi na wahamiaji duniani, lakini makubaliano hayo yaliyofikiwa mwaka jana, yanakinzana na sera za marekani kuhusu uhamiaji na wakimbizi chini ya utawala wa trump.