UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI

 

Jumla ya kaya maskini 147  katika shehia ya kijini makunduchi  zinanufaika na mradi wa kujiimarisha  na  kuongeza kipato kufuatia  utekelezaji wa mpango wa  kunusuru kaya maskini tasaf awamu ya tatu wenye lengo la kuwawezesha walengwa hao kuondokana na umaskini uliokithiri.

Wakizungumza  katika ziara  ya  kukagua  mradi wa ajira za muda kwa wanakaya maskini  iliyofanywa na kamati ya uongozi ya tasaf unguja,wasimamizi wa mradi huo  wamesema  pamoja na mafanikio wanayopata katika uendeshaji  wa  vitalu vya miti ya kudumu na ya matunda  bado wanakabiliwa na tatizo la ufinyu wa soko la  kuiuza  miti hiyo ambayo katika hatua za awali wamekuwa wakiuziana  walengwa  na kuweza kupanda katika maeneo yao.

Kamati hiyo  ya uongozi ya tasaf  imesema  tasaf imo katika jitihada za kuwapatia soko kwa kuisambaza miti hiyo katika maeneo mbalimbali inayohitaji  kupandwa miti ili kuweza kusaidia  kuondoa tatizo hilo kwa walengwa hao na pia kupunguza  uharibifu wa mazingira uliopo.

Mapema kamati hiyo ilipokea ripoti ya robo ya  tatu ya  mwaka  2016-2017   ambayo  imeelezea mfanikio kadhaa ikiwemo kuwajengea uwezo walengwa katika kuzijua fursa za kutekeleza miradi yao