UTEKELEZAJI WA SUALA LA MIPANGO MIJI KATIKA UKANDA WA PWANI

 

 

Mkurugenzi mipango miji  na vijiji dr mohammad juma amesema  katika utekelezaji wa suala la mipango miji katika ukanda wa pwani idara  tayari   imeanza  na  hatua za ukusanyaji wa maoni ya wananchi juu ya  mahitaji muhimu wanayotaka  yazingatiwe  wakati  wa  ujenzi wa  miji hiyo.

Akizungumza  kwa nyakati  tofauti  na wakaazi  wa marumbi na uroa  dk  muhammad   amesema   ujenzi wa  mpango  huo  utazingatia zaid mambo muhimu ambayo  yalifeli katika  mpango wa awali ulioundwa mwaka 1995  yakiwemo maeneo  ya wazi baina ya jengo na jengo ambayo yameonekana kutumika.

Wakitoa maoni yao  wakaazi hao  wamezitaka  taasisi  zinazoshughulikia  masuala ya ardhi  kujenga ushirikiano   katika kutekeleza  kazi  hizo  kwani kutokufanya hivyo ni moja ya  sababu inayochangia  kutoendelea vizuri mipango  inayopangwa.

Hatua hiyo  ya mkakati wa matumizi ya ardhi  inatarajiwa kukusanya maoni ya wakaazi  wa  shehia  tisa  za  kanda ya ghuba  ya  chwaka   matemwe.