UTENDAJI WA SHIRIKA LA BANDARI LICHA YA MATATIZO LINAYOKABILIANA NAYO

 

 

Kamati ya ardhi na mawasiliano ya  baraza la wawakilishi zanzibar imesema  imeridhishwa na utendaji wa shirika la bandari licha ya matatizo linayokabiliana  nayo.

Imesema  shirika hilo muhimu kiuchumi linafanya kazi kwa bidii kubwa ingawa baadhi ya changamoto zake ziko nje ya ewezo wake.

Kauli iyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo mhe, hamza hassan juma   katika ziara ya  kamati yake ilipotembelea   shirika la bandari na kusema linajenga matumani mazuri kwa serikali.

Amesema miongoni mwa changamoto zinazolikabili shirika ni pamoja na  shirika kukosa malipo  ya minara   kutoka kwa shirika la bandari  la jamhuri ya muungano wa tanzania pamoja na  kukosa hati miliki ya minara  hiyo inayoongozea vyombo vya baharini.

Naibu waziri wa mawasiliano na usafirishaji mhe, mohd ahmada amesema  mrundikano wa makontena katika  bandari ya malindibado ni tatizo huku kasi ya ya ukuaji wa ikiendelea kukuwa kupitia bandari hiyo.

Mkuregenzi mkuu wa shirika la bandari zanzibar capt, abdalla juma  amesema tatizo la msongamano mkubwa wa makontena unaosababisha usumbufu limo katika hatua za kupatiwa ufumbuzi.