UTETEZI NA USHAWISHI KWENYE MASUALA YANAYOWAGUSA WATU WENYE ULEMAVU SERIKALINI

Umoja wa watu wenye ulemavu zanzibar (uwz) umetakiwa kufanya utetezi na ushawishi kwenye masuala yanayowagusa watu wenye ulemavu serikalini ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa katika mipango yao yanaendelea badala ya kufanyiwa na watu wengine.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa umoja wa watu wenye ulemavu zanzibar mkuu wa mkoa wa mjini magharibi mh. Ayoub moh’d mahmoud katika mkutano wa kuchagua viongozi wapya watakao ongoza katika miaka minne katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kikwajuni weless. Amesema ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa katika kuanzisha hna kutekeleza na kutathmini mipango ya maendeleo. Hivyo kushiriki na kushirikishwa kwao katika mchakato huo mzima kutaijenga jamii shirikishi ambayo watu wenye ulemavu watapata haki na fursa sawa.
Mkurugenzi mtendaji wa umoja huo bi asia ali hussein amesema mbali na mafanikio waliyoyapata na jumuiya imefanikisha lakini bado wanakumbana na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeleza program zao kama utoaji wa elimu.
Baada ya hapo umoja wa watu wenye ulemavu walifanya uchaguzi wa kuchagua viongozi watakao waongoza kwa kipindi cha miaka minne katika ukumbi wa watu wenye ulemavu ambapo waliwachagua mwenyekiti bi salma makame mwenyekiti haji saadati ali omar makame katibu mkuu nassor suleiman nassor pamoja na mshika fedha na wajumbe wa halmashauri kuu.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa mwenyekiti bi salma saadat amesema atashirikiana na jumuiya zote za watu wenye ulemavu katika kuleta maendeleo yao.
Kaimu wa bodi ya wadhamini bwana hamza zubeir rijali amesema uchaguzi umeenda vizuri na kwa vile watu wenye ulemavu wameshirikishwa katika uchaguzi wao walio wataka.