UTIAJI SAINI WA MPANGO MKUU WA MATUMIZI YA ARDHI

Changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika maeneo ya zanzibar yamesababisha kufanyiwa mabadiliko ya mfumo wa matumizi ya ardhi ili kuenda sambamba na ongezeko la idadi ya watu na mipango ya kuichumi na kijamii.
Mkurugeni wa mipango miji na vijiji dk. Mohamad juma akizungumza katika utiaji saini wa mpango mkuu wa matumizi ya ardhi mkoa wa mjini magharibi ametaja matatizo hayo ni kutokuwa na ujenzi endelevu, ambapo matumizi ya ardhi ni makubwa ikilinganishwa na idadi ya watu ambapo hadi kufikia mwaka 2030 idadi ya wakaazi katika mkoa huo inakadiriwa kufikia watu milioni moja na nusu.
Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi mh. Ayoub mohamed mahmoud amesema serikali imeweka utaratibu maalum wa kuwashirikisha wananchi katika mipango yake mbalimbali, hivyo kila taasisi iwajibike kuhakikisha mpango mkuu wa mji unafanikiwa ili kufikia matarajio.
Akiuzngumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya wenzake mkuu wa wilaya ya mjini marina joel thomas mpango huo utatoa fursa nzuri ya matumizi bora ya ardhi kwa faida ya vizazi vijavyo.
Mkuu huyo wa mkoa alisaini mpango huo pamoja na kuukabidhi kwa wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa manispaa za mkoa wa mjini magharibi ili upelekwe kwa wananchi na kutoa maoni yao na baadae urejeshwe serikali kwa utekelezaji.