UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU NA NYARAKA NI NYENZO MUHIMU KWA SERIKALI NA TAIFA

 

Suala la utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika taasisi za serikali imeelezwa kuwa ni nyenzo muhimu kwa serikali na taifa kwani ni muhimu katika kufanya marejeo .

Mkurugenzi taasisi ya nyaraka na kumbukumbu ndugu salum suleiman ameeleza hayo katika maafunzo maalum ya utunzaji na usimamizi wa kumbukumbu kwa masheha wa wilaya ya magharibi “b” yenye lengo la kuwawezesha masheha  kuwa na utunzaji mzuri wa kumbukumbu wanazozizalisha katika ofisi zao na kubaki salama

Amesema taasisi za umma ni muhimu kuwa na sehemu ya kutunza kumbukumbu kwani ripoti inaonesha kuwa taasisi nyingi za umma katika suala la utunzaji wa kumbukumbu sio wa kiridhisha hali inayosababisha kupotea kwa   baadhi ya kumbukumbu  muhimu katika ofisi.

Afisa wa kumbukumbu katika idara ya nyaraka ndugu fuad abdallah amesema kumbukumbu ni hazina  kwa serikali mbali ya kuwa nyenzo ya shughuli za utawala  pia husaidia kuimarisha umoja , uzalendo , utaifa na kujenga misingi imara ya utawala bora.

Katika hatua nyengine masheha wamesema mafunzo hayo yatawaletea mabadiliko katika kazi zao licha ya kuwa na changamoto ya vifaa vya utendaji kazi.