UWEZEKANO WA KUPUNGUZA GHARAMA ZA KUAGIZA MBEGU KUTOKA NCHI NYENGINE

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema upo uwezekano mkubwa wa kupunguza gharama za kuagiza mbegu kutoka nchi nyengine kwa ajili ya wakulima kutokana na hali halisi ya mavuno yanayopatikana na wakulima hao.
Akizindua shughuli za uvunaji wa mpunga unaofanywa na wakulima wa bonde la bumbwisudi,kufuatia mbegu ya ukulima unaotumia maji kidogo na mbegu kidogo na kupata mavuno mengi (shadidi) , waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mh.hamad rashid amesema ni vyema wakulima kutumia mbinu bora zitakazowawezesha kupata faida kubwa ya kazi yao,kwa kuweka mavuno wanayopata pamoja na kueka asilimia ya mbegu wanayohitaji ili kuepusha uzoefu wa kuagiza mbegu kutoka nje ya zanzibar.
Mkuu wa bonde la umwagiliaji maji bonde la bumbwisudi kadir ali kadir amesema mfumo huo wa ukulima wa shadidi unaleta faida kubwa hassa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabianchi.
Nao wakulima hao wameiomba serikali kuwapatia eneo kubwa zaid la kuendeleza shughuli zao za kilimo ili kuongeza faida kwao na taifa kwa jumla.
Jumla ya heka mbili za ukulima wa mpunga unaotumia mbegu kidogo mavuno mengi umelimwa na wakulima wa kikundi cha awezeshae ni mola cha bumbwisudi.