UZALISHAJI WA BIDHAA ZA MAZIWA UNAOTEGEMEA MALIGHAFI

 

Kampuni binafsi zinao mchango mkubwa wa kuzinufaisha jamii za wakulima na wafugaji nchini kutokana na uzalishaji wa bidhaa zao unaotegemea malighafi kutoka kwa jamii inayoizunguka.

Kama amabvyo kampuni ya tanga fresh ilivyotoa fursa ya umiliki wa asilimia 40 ya hisa kwa vyama vya ushirika vya wafugaji

Kauli hiyo imejidhihirisha pale zbc iilipotembelea kampuni ya maziwa ya tanga frsh kanda ya dar-es-salaam ambapo meneja masoko wa kampuni hiyo ally sechonge alisema  mahitaji halisi ya maziwa ni lita laki moja na ishirini kwa siku wakati kwa sasa wanapata lita 48 hadi 50 elf tu.

Kuhusu nafasi ya maziwa ya tanga fresh kwa familia na jamii ndugu sichonge akaelezea hatua nne za vigezo vinavyotumika kupokea maziwa kutoka kwa wafugaji kuwa ni pamoja na kuhakiki hali ya usafi, uzito wa maziwa ,kipimo cha maji na kuangalia ladha ya uchachu.

Maziwa ya tanga fresh yanakidhi viwango vya kimaifa na kuweza kuwa sehemu ya lishe na burudani kwa wageni wanaokuja nchini wakiwemo watalii