VIJANA KUACHANA NA VITENDO VIOVU NA BADALA YAKE KUFANYA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI

Mkuu wa wilaya mjini ndugu marina joel thomas, amewataka vijana kuachana na vitendo viovu na badala yake kujihamasiha katika shughuli za uzalishaji mali zenye tija kwao na taifa kwa jumla.
Akifungua mafunzo ya mfumo wa taarifa za soko la ajira kwa mabaraza ya vijana wilaya ya mjini, amesema zanibar imo katika ramani ya kuwa na idadi ndogo ya uwepo wa tatizo la ukosefu wa ajira kutokana na fursa mbalimbali ziliopo ndani ya nchi.
Aidha amefahamisha kwamba kilio kiliopo cha ukosefu wa ajira kinatokana na kutoelewa mbinu na utafutaji wa soko hilo hivyo kufuatia mafunzo hayo vijana watafaidika na kupata uelewa wa upatikanaji wa ajira.
Nao vijana washiriki wa mafunzo hayo wamesema pamoja na matatizo yanayowakabili lakini baada ya kuanzishwa kwa mabaraza ya vijana kumekuwepo kwa mabadilko ya kifikra hasa katika nyanja za kiuchumi miongoni mwao.
Wakizungumzia kuhusu vijana kujiunga katika mabaraza hayo wamesema changamoto kubwa ipo kwa vijana wa kiume ambao wengi hawajahamasika ikilinganishwa na vijana wa kike.