VIJANA KUBUNI MBINU TOFAUTI AMBAZO ZITAWAPA AJIRA

Jitihada za makusudi kwa vijana zinahitajika katika kupambana na maisha na kubuni mbinu tofauti ambazo zitawapa ajira na kuwaingizia kipato.
Hayo yanaonekana kwa vijana ambao ni wajasiriamali wa mradi wa mkaa unaotokana na mapumba ya miwa na majani takataka waliopo kiembesamaki, ambapo wamesema ipo haja ya serikali kutoa msaada kwa vijana ili waweze kujiajiri wenyewe.
Nao wanunuzi wa mkaa huu wamesifu ubora wa mkaa huo ambapo wamewasisitiza wananchi wenzao kuununua ili kuepuka na gharama zisizo za lazima.
Malighafi wanayotumia vijana hawa kuzalisha makaa hayo, ni moja kati ya msaada mkubwa wa kuweka mazingira safi katika manispaa mbalimbali za hapa zanzibar.