VIJANA KUJIANDAA KITAALUMA ILI KUZITUMIA FURSA ZA SOKO LA PAMOJA LA MTANGAMANO

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid amewataka vijana kujiandaa kitaaluma ili kuzitumia fursa za soko la pamoja la mtangamano wa afrika mashariki katika kuzalisha ajira kupitia njia mbali mbali za kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ametowa wito huo Madungu wakati akifungua mafunzo ya elimu kuhusu DIASPORA  kwa wajumbe wa mabaraza ya vijana na kusema kuwa serikali imedhamiria kutanua shughuli za kiuchumi kwa wananchi wake kupitia mtangamano huo pale utakapoanza utekelezaji wake.

Muwezeshaji wa mafunzo hayo Ali Ameir Haji Afisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Wazanzibara wanaoishi Nje ya Nchi  amesema azma yao ni kuanzisha mashirikiano baina ya mabaraza ya vijana na  wanadiaspora hao ili kuondosha changamoto zao.

Kwa upande wa vijana hao wameriki kwamba mtangamano huo wa Afrika Mashariki una fursa nyingi zinazoweza kuwakombowa vijana kiuchumi.