VIJANA KUSOMEA MASUALA YA UTABIBU ILI KUPUNGUZA UHABA WA WATAALAMU

Daktari dhamana wa wilaya ya kaskazini “a” himid juma said amezungumzia haja kwa vijana wa wilaya hiyo kusomea masuala ya utabibu ili kupunguza uhaba wa wataalamu katika vituo vya afya.
Akizungumza baada ya kupokea msaada wa mashine ya ultra sound kutoka kwa shirika la mia la italia kwa ajili ya kituo cha afya cha pwani mchangani himid amesema ingawa wamepata msaada wa mashine hiyo lakini kuna changamoto ya kutokuwa na wataalamu wanaojua kuitumia.
Amesema kupatikana kwa mashine hiyo kutaondoa kilio kwa akina mama cha kufuata huduma hiyo ya mashine hiyo katika hospitali ya kivunge umbali wa meli tisa kutoka pwani mchangani.
Wakitoa shukrani zao kwa shirika la mia wakaazi wa pwanimchangani wamesema wamefaidika na msaada huo kwani walikuwa wanafuata huduma hiyo mbali jambo ambalo lilikuwa linawasababishia kutofanya shughuli zao nyengine za maendeleo.
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika hilo hapa tanzania ndugu mohamed ali amesema wametoa msaada huo pwani mchangani baada ya kuona akina mama wanapata taabu na madaktari kuitumia vyema.