VIJANA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTANGAZA MAENDELEO YA MABARAZA BILA YA KUPOTOSHA

 

Makamu wa Rais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Samia Suluhu Hassan, amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kutangaza maendeleo ya mabaraza yao bila ya kupotosha.

akizindua baraza la vijana la zanzibar amesema ili kujenga mabaraza imara  katika utekelezaji wa kazi zake, ni fursa nzuri ya kutumia mitandao hiyo ili kila mmoja afahamu na kuweza kuzidisha idadi ya  vijana ndani ya mabaraza yao.

Mh. Samia amesema  idadi  ya vijana katika kujiunga na mabaraza hayo bado hairidhishi ikilinganishwa na idadi ya vijana waliopo zanzibar, hivyo amewataka  kutafakari  na kutoa elimu ili kuongeza kasi ya vijana kujiunga.

Akizungumzia suala la udhalilishaji kwa wanawake na watoto makamu wa rais amewakumbusha vijana kuwa wasimamizi wazuri katika kupinga vitendo hivyo ambavyo vinaathiri ustawi wa watoto huku akiwasisiza watendaji wa  taasisi zinazotoa huduma za kisheria kutekeleza majukumu yao ili kumaliza tatizo hilo.

Mwenyekiti wa baraza la vijana zanzibar. Nd. Khamis kheri, akisoma risala amesema bado wanakambiliwa na changamoto ya ukosefu wa jengo la ofisi ya kuweza kufanya kazi zao kwa urahisi.

Waziri wa kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto mh. Moudline castico na katibu mkuu wa wizara hiyo. Nd. Fatma gharib wamesema pamoja na matatizo yaliyo ndani ya baraza hilo watahakikisha wanazisimamia ili fursa zaidi zipatikane.