VIJANA KUYATUMIA MABARAZA YA VIJANA KUFIKISHA MAAMUZI YAO

 

Kamishna wa kazi zanzibar bi fatma idd amewataka Vijana kuyatumia mabaraza ya vijana kufikisha Maamuzi yao  ili waweze kusikika mahitaji yao.

Akizungumza  katika kongamano  la vijana liloandaliwa na jumuia ya wanasheria wanawake zanzibar (zafela) kupitia mradi wa paza sauti amesema vijana  ni tegemeo kubwa la taifa la kesho hivyo ni vyema wakapewa nafasi ya kuzungumzia  matarajio yao.

Bi fatma amesema  vijana  wamekuwa wakitumiliwa katika ngazi mbalimbali  lakini wamekosa kutimiza malengo yao licha ya kuwepo kwa fursa nyingi ambazo hawafaidiki nazo kwa vile sauti zao hazisikiki.

mkurugenzi wa zafela  jamila mahamoud, amesema kuwa lengo la kuewpo mradi huo ni kuona vijana wanashirikishwa katika ngazi mbalimbali na kuona tatizo la ajira linaondoka kwao iwapo watajiingiza katika kazi za ujasiriamali

nao washirki wa kongamano hilo nd habiba suleiman na khamisi ali, wamesema kongamano hilo limewapa ujasiri wa kujiamini katika kuzitumia fursa za ajira zilizopo ili kufikia malengo waliojiwekea  kongamano hilo la siku moja kwa vijana  limetoa mada mbali mbali zinazowahusu vijana na kutoa maoni yao .