VIJANA NCHINI KUITUNZA AMANI ILIOPO NA KUACHANA NA TABIA YA KUJIINGIZA KATIKA VURUGU.

 

Naibu waziri wan chi ofisi ya rais tawala za mikoa idara maalum za smz mh samata shaame khamis amewataka vijana nchini kuitunza amani iliopo na kuachana na tabia ya kujiingiza katika vurugu.

Mh shaamata akizungumza na vijana katika uzinduzi wa thamthilia mbili   zenye maadili mema kwa vijana hapo malindi mh samata amesema vurugun zinapoteza maendeleo  kazi na mapato ya nchi hivyo ni vyema kila mmoja kuangalia maisha bora yenye utulivu na amani.Hata hivyo shamata amewataka vijana kuwaelilimisha vijana wenzao katika kutafuta mbinu na za kuteta maendeleo endelevu na kutojiingiza katika vitendo hatarishi.Muanzilishi wa kituo cha majadiliano ya vijana nd hashim pondeza amesema lengo la taasisi yake ni kuweza kuwakumbusha jamii jinsi ya kupokea habari zilizo bora na imara katika mitandao ya kijamii na kuachana kujiingiza katika vishawishi