VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUVITUMIA VITUO VYA HUDUMA RAFIKI KWA VIJANA

 

 

Wito huo umketolewa na waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mh,Hamad Rashid Mohammed wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya wete huko bwagamoyo mtambwe katika uzinduzi wa kituo cha huduma rafiki kwa vijana ikiwa ni sehemu ya  shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar.

Amesema uwepo wa vituo vya huduma rafiki kwa vijana ni njia moja ya kuwasidia kuondokana na matatizo kwani kwa sasa kumeonekana kubadilika kwa mila na desturi kitu ambacho kinawapelekea vijana kujisahau.

Akizungumzia suala la mapinduzi ya zanzibar mh, hamad rashid amesema kuna kila sababu ya kuyaenzi na kuyathamini kwani ndio mkombozi wa wazanzibari na yamejikita kuwaletea maendeleo.

Naye afisa mdhamini wizara ya afya nd, bakari ali bakari amesema ujenzi wa vituo vya huduma rafiki kwa vijana umekuja ili kuwasaidia vijana kupata mafunzo ya kujiepusha na tabia hatarishi.

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa kaskazioni pemba mh,omar othman khamis amewataka vijana kuwa mfano mwema kwani wao ndio tegemeo la taifa.