VIJANA WAMEANZA KUBADILIKA KIMTAZAMO

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema vijana wameanza kubadilika kimtazamo wa kuacha utegemezi hali itakayosaidia kuondosha tatizo la ukosefu wa ajira zanzibar.
Afisa uweseshaji zanzibar zena seif hamad amesema mafanikio hayo yanatokana na mikakati mingi ya kuliendeleza kundi hilo kwa kushirikiana na taasisi mbalimabali katika kuwaendeleza kiuchumi.
Akizungumza katika mkutano wa kujadili muongozo wa ajira kwa vijana amesisitiza kuangaliwa taaluma za fani nyengine zinaweza kutumiwa kama njia ya kujiajiri kwa kundi hilo.
Katibu mtendaji wa jumuiya ya kukabiliana na changamoto za vijana walioandaa mpango huo zafyco abdalla abeid amesema ramani hiyo itaanza kuangalia fursa nyingi kwa mujibu wa maeneo na anaamini itaondoa mkwamo wa ajira kwa vijana.
baadhi ya vijana walioshiriki kongamano hilo wameshauri serikali kuwasaidia kuweka mipango bora pamoja na kusikiliza vijana katika kupanga mikakati yakuwaendeleza kielimu na kiuchumi