VIJANA WAMESISITIZWA KUWA WASIMAMIZI WAKUU WA KUPAMBANA NA VITENDO VYA RUSHWA

Mkuu wa wilaya ya mjini bi : marina jeol thomas amewasisitiza vijana kuwa wasimamizi wakuu wa kupambana na vitendo vya rushwa ili nchi iweze kupiga hatua katika maenedeleo
Akizungumza katika mafunzo ya kupambana na rushwa kwa vijana wa wilaya ya mjini bi marina amesema rushwa inapaswa kupigwa vita kwani inachangia ukiukwaji wa haki na kuleta vurugu nchini.
Amefahamisha kuwa vijana mara nyingi hutumika katika masuala tofauti hivyo wanapaswa kujitambua ili kupambana na vitendo vitokanavyo na rushwa.
Kwa upande wake afisa elimu wa mamlaka ya kuzuia na kubambana na rushwa bw mussa omar amesema kukithiri kwa rushwa kunatokana na kuporomoka kwa maadili hivyo kuna umuhimu wa kutolewa elimu katika ngazi za chini ili kuweza kuliondosha tatizo hili.
Nao vijana wa mabaraza hayo wamesema ni vyema wakapatiwa elimu zaidi ili waweze kubadilika na kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya rushwa