VIJANA WAMETAKIWA KUIPA KIPAUMBELE SEKTA YA KILIMO AMBAYO INA FURSA NYINGI ZA AJIRA

Vijana wametakiwa kuipa kipaumbele sekta ya kilimo ambayo ina fursa nyingi za ajira na inaongeza uzalishaji wa chakula.
Waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi mh. Hamad rashid mohamed amesema katika kuhakikisha sekta hiyo inapiga hatua wizara inatoa taaluma na kushajihisha vijana kulima kilimo chenye tija kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya chakula duniani yatayokwenda sambamba na maonyesho ya kilimo dole-kizimbani amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kupata utaalamu na maelekezo kuhusu masuala ya kilimo ili kuleta mageuzi ya kimaendeleo kupitia sekta hiyo.
Mratibu wa maonyesho hayo othman ali maulid amesema fursa nyingi muhimu zitapatikana ikiwemo elimu ya kilimo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kila siku.
Kamishna wa chuo cha mafunzo zanzibar ali abdalla ali amesema kuna haja kwa jamii kubadili mtazamo na kuipa umuhimu sekta ya kilimo ambapo teknoloji ayake imekuwa.
Waziri hamad pia amepata fursa ya kutembelea eneo la kudumu litakalofanyika maonyesho huko kizimbani ambalo liko katika hatua ya matayarisho.