VIJANA WATAKIWA KUONDOSHA DHANA YA KUONA KUWA KAZI YA KILIMO NI YA WATU WA VIJIJINI

Waziri wa biashara na viwanda, balozi Amina Salum Ali, amewataka vijana kuondosha dhana ya kuona  kuwa kazi ya kilimo ni ya watu wa vijijini.

Balozi Amina amesema kilimo hasa kinachozingatia maelekezo  ya  kitaalamu kimekuwa ni mkombozi mkubwa wa  maisha ya watu walioamua kujikita katika sekta hiyo ikiwemo kilimo cha mboga mboga ambacho kimekuwa na tija, hivyo amewataka vijana  kuelekeza nguvu zao ili waweze kujiimarisha kiuchumi.

Akifunga mafunzo ya miezi mitatu ya kilimo hai kwa maendeleo endelevu, kwa vijana 18  balozi Amina amesema serikali imekuwa katika jitihada za kuhakikisha vijana wanajiimarisha katika ujasiriamali na kuwajengea mazingira bora ya kuwapatia fedha za mkopo waweze kuendesha vyema shughuli zao za kujitegemea.

Wafadhili wa mafunzo hayo taasisi ya kuongeza kasi ya maendeleo Zanzibar milele Zanzibar foundation, katika taarifa iliyomwa na afisa maendeleo, biashara na uchumi jamii, Nd. Ghalib Khamis Machano, amesema wanawakaribisha wafadhili kuwasaidia vijana waliopata mafunzo ili kuitumia vizuri taaluma waliyoipata ya kilimo hai.

Mratibu wa fursa kijani iliyoendesha mafunzo hayo, bi Agnes  Bweye, ameelezea umuhimu wa taaluma hiyo ya kilimo hai, ambapo risala ya wahitimu iliyosomwa na Kassim Maulid imependekeza maombi ya kuwezesha vijana hao kuweza kujiimarisha katika ujasiriamali.

 

 

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App