VIJIJI VYA HIFADHI YA BAHARI YA GHUBA YA MINAI VIMEIOMBA SERIKALI KUWAPA MGAO WA FEDHA

Vijiji vilivyomo ndani ya hifadhi ya bahari ya ghuba ya minai vimeiomba serikali kuwapa mgao wa fedha zinazotokana na utalii kama zinavyotolewa kwenye vijiji tisa vinavyohusiana na hifadhi ya msitu wa jozani.
Ombi hilo limetolewa na wakaazi wa vijiji vya kizimkazi na kikungwi wakati wakizungumza na zbc kwa nyakati tafauti na kuifikisha kero hiyo kwa mkuu wa wilaya ya kati.
Wamesema mradi wa minai umeshindwa kuwajengea uwezo na kuwainua kimaisha wananchi waliozungukwa na raslimali ya bahari katika ukanda huo zilizowekwa katika hifadhi
Wamesema wakati wa kuanzishwa kwa mradi huo wa minai ilitoa vifaa vichache ambavyo havikutosha kulingana na mahitaji ya wavuvi na sasa taasisi hiyo inajihusisha zaidi na vibali vya watalii bila ya kufikisha mapato hayo kwa wanakijiji.