VIKOSI VYA IRAQ VIMEFANIKIWA KUKOMBOA ASILIMIA 30 YA ENEO LA MAGHARIBI LA MJI WA MOSUL NCHINI HUMO

Vikosi vya iraq vimefanikiwa kukomboa asilimia 30 ya eneo la magharibi la mji wa mosul nchini humo kutoka kwa kundi la islamic state is.

Kundi hilo kupoteza mji wa mosul ni pigo kubwa kwani ni ni mji mkubwa kabisa waliokuwa wakiudhibiti  tangu mwaka 2014.

Kiasi ya raia wapatao laki sita  wanakadiriwa kukwama ndani ya mji wa mosul huku wengine laki mbili wamepoteza makaazi yao tangu kuanza kampeni ya kuukomboa mji huo mwezi oktoba.

Wakati huo huo balozi wa marekani brett mcgurk anaehusika kuongoza operesheni ya pamoja na ya majeshi dhidi ya wapiganaji wa islamic state amesema watawau wapiganaji wote wa kundi hilo waliosalia mjini mosul.