VIKOSI VYA JESHI LA KOREA YA KUSINI VIMEANZA LUTEGA ZA PAMOJA ZA NDEGE ZA KIJESHI

Vikosi vya jeshi la korea ya kusini na vile vya marekani vimeanza lutega za pamoja za ndege za kijeshi.
Luteka hizo zinasemekana kuwa kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa zikiwa na ndege 230 za kivita za marekani na wanajeshi elfu 12 wanashiriki katika luteka hizo zilizopewa jina “vigilant ace”.
Luteka hizo za siku tano zimelengwa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
November mwaka jana wanajeshi elfu 16 na zaidi ya ndege za kivita mia mbili zilishiriki katika luteka hizo zinazofanyika kila mwaka.
Siku chache zilizopita korea ya kaskazini ilifanya jaribio la kombora la kinyuklia lenye uwezo wa kushambulia bara moja hadi jengine, jaribio lililolaaniwa ulimwenguni kote.
Viongozi wa mjini pyongyang wanaituhumu marekani, luteka zake za kijeshi pamoja na korea ya kusini zimelengwa kuandaa hujuma dhidi yake. Viongozi wa korea ya kusini na marekani wanakanusha tuhuma hizo.