VIKOSI VYA USALAMA NCHINI PHILIPPINES VIMEDHIBITI KARIBU ENEO LOTE

Vikosi vya usalama nchini philippines vimedhibiti karibu eneo lote la mji wa kusini wa marawi ambapo wapiganaji wenye uhusiano na kundi la dola la kiislamu wameanzisha mapigano ya umwagaji damu wiki moja iliyopita.
Hata hivyo hofu imeongezeka kwa raia kushindwa kukimbia mapigano katika mji huo.
Habari zinasema kuwa raia 24 ni miongoni mwa waliouwawa katika mapigano hayo kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji hao.
Juhudi za kusaidia kuwaokoa raia waliokwama kwenye mji huo wenye mapigano zinafanyika ambapo inadaiwa kuwa zaidi ya raia elfu 2 bado wamekwama huku wakiomba msaada wa chakula.