VIONGOZI AMBAO NI WATUMISHI WA UMMA WAMETAKIWA KUWA WAKWELI

 

 

Viongozi ambao ni watumishi wa umma wametakiwa kueleza  ukweli  wakati  wa  kujaza fomu za mali madeni  ili kuondoa mgongano wakati wa ufatiliaji.

kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma ndugu Assa Hamadi Rashid wakati akizungumza katika mkutano  na wahasibu, wakaguzi wa ndani na nje wa wizara na taasisi za serikali, ulofanyika katika ukumbi wa idrssa abdulwakil uliopo manzi mmoja mjini unguja,

amesema wengine hudiriki kusema uwongo kwa kuhofia kuchukuliwa hatua za kimaadili wakti sheria haikatazi kumiliki mali wala kuwa mfanya biashara tatizo.

katibu wa tume ya maadili ndugu kubingwa mashaka simba akizungumza katika mkutano wa maadili ya viongozi uliofanyika ukumbi wa bima, mpirani, na kushirikisha majaji mahakimu na makadhi  amewataka kuwa waadilifu katika umiliki wa mali zao  ili kuondoa hofu wakati wakujaza fomu.

washiriki walipata fursa ya kutoa maoni, ushauri na maswali ambayo yote yalipatiwa majibu yake.