VIONGOZI WA MADAKTARI KENYA WAACHILIWA HURU.

https://youtu.be/VAtDe8lb3Dg

 

Mahakama ya rufaa nchini kenya imeamua viongozi wa chama cha wahudumu wa afya waliokuwa wamefungwa jela mwezi mmoja waachiliwe huru.

Viongozi hao saba walifungwa jumatatu baada ya kupatikana na hatia ya kutofuata uamuzi wa mahakama wa kumaliza mgomo wa madaktari ambao umedumu kwa zaidi ya miezi miwili.

Viongozi hao wametakiwa kuhakikisha suluhu ya mgomo huo inapatikana katika kipindi cha siku saba.

Mazungumzo ya kutafuta suluhu yataongozwa na chama cha wanasheria kenya (lsk) na tume ya kitaifa ya haki za kibinadamu (knhcr).