VIONGOZI WA MADAKTARI KENYA WAFUNGWA JELA MWEZI MMOJA

 

Mahakama ya   wafanyakazi nchini kenya imewahukumu kifungo cha mwezi mmoja viongozi saba wa chama cha wahudumu wa afya (kmpdu) kwa kukaidi agizo la kumaliza mgomo uliodumu kwa zaidi ya miezi miwili.

Karibu madaktari na wauguzi 5000 kutoka hospitali 2000 za umma, walianza mgomo wiki ya kwanza ya mwezi desemba na wagonjwa wamekuwa wakikosa matibabu ili kushinikiza serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara

Jaji hellen wasilwa amesema viongozi hao hawajatoa sababu ya kutosha za kuonesha sababu ya kutomaliza mgomo huo baada ya muda wa wiki mbili na nusu kumaliza mgomo huo