VIONGOZI WA SERIKALI WALIOBADILISHANA MAENEO KUFANYA KAZI KUJENGA MASHIRIKIANO

 

Katibu mkuu afisi ya makamo wa pili wa rais dr, Idrissa Muslim  Hija amewataka viongozi wa serikali waliobadilisha maeneo yao ya kufanya kazi kujenga mashirikiano na wafanyakazi katika afisi hizo mpya.

Dr, Idrisa ameeleza hayo katika hafla ya makabidhiano ya afisi kati yake na mkuu mpya wa mkoa kusini unguja hassan khatib hassan huko tunguuu.

Amesema malengo ya serikali hayawezi kufanikiwa endapo viongozi na watedaji wengine hawatakuwa na ushirikiano.

Wakati huo huo naibu katibu mkuu wizara ya kazi unayeshughulikia wazee, vijana ,wanawake na watoto bi mwanajuma majid abdalla amezungumzia haya ya kuongezwa kasi ya mapambano dhidi tya udhalilishaji ili kkomesha kabisa vitendo hivyo.

Ameeleza hayo mwanakwerekwe wakati wa makabidiano ya afisi kati yake na aiyekuwa akishikilia nafasi hiyo mhe hassan khatib hassan ambae sasa ni mkuu wa mkoa kusini unguja.

Hafla hiyo pia iliyohudhuriwa na waziri wa uwezeshaji wanawake na watoto mhe modline castrico na naibu waziri wake mhe shadya moh’d suleiman.