VIONGOZI WA TAASISI KUSIMAMIA VYEMA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

 

 

Mkuu wa wilaya ya mjini bi marina joel thomas amewataka viongozi na taasisi mbalimbali kusimamia vyema fedha za miradi ya maendeleo wanazopatiwa na wahisani mbalimbali ili kuleta tija kwa jamii.

Akizungumza katika ghafla maalum ya kukabidhi cheki za fedha zenye thamani ya shilingi milioni tano kwa miradi kumi ya maendeleo iliyopitiwa na mwenge wa uhuru 2017 ndani ya wilaya ya mjini

Bi marina amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ofisi yake itafatilia kwa karibu matumizi hayo na endapo matumizi hayo yataenda kinyume na makubaliano hatua za kisheria zitachukuliwa .

Wakitoa shukrani kwa niaba ya wenzao wameishukuru ofisi ya mkuu wa wilaya  kwa kuwapatia msaada huo kwani utasaidia kutotu changamoto znazowakabili.

Aidha wameiomba afisi hiyo kuendelea na utaratibu huo wa kutoa misaada jambo ambalo litaleta manufaa kwa umma.