VIONGOZI WA URUSI, UTURUKI NA IRAN WAMEKUTANA KATIKA MJI WA UTALII WA SOCHI

 

Viongozi wa urusi, uturuki na iran wamekutana katika mji wa utalii wa sochi ulio katika mwambao wa bahari nyeusi, kujadiliana juu ya mpango wa amani wa kumaliza vita nchini syria.

Masuala yaliyozungumzwa ni pamoja na kuwarejesha nyumbani wakimbizi, msaada wa kibinadamu na kubadilishana wafungwa kati ya pande zinazohasimiana.

Wakati huo huo upinzani wa syria uliogawanyika umekutana nchini saudi arabia katika juhudi za kusuluhisha tofauti zao na kuwa na msimamo mmoja katika mazungumzo ya amani mjini geneva.

Rais wa urusi vladimir putin amesema suluhisho la amani litahitaji maridhiano na kujitolea kwa kila upande, ikiwemo serikali ya rais bashar al-assad.

Akizungumza baada ya mkutano huo wa nchi tatu, putin amesema rais wa syria ameahidi mabadiliko ya katiba na kuendesha uchaguzi ambao utasimamiwa na umoja wa mataifa.