VIONGOZI WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAAMA KUHAKIKISHA HALI YA USALAMA KWA WANANNCHI

Waziri wa nchi wa makamo wa pili wa raisi mohamed aboud mohamed amewataka viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalaama na watendaji wa mkoa wa kaskazini a na b unguja pamoja na masheha kuhakikisha hali ya usalama kwa wanannchi na raiya wanaotoka nje ya nchi ili kudhibiti mali zao katika mkoa huo pamoja na wilaya hiyo.
Wito huo umetolewa wakati akifanya mazungumzo na watendaji mbali mbali wa serikali katika chuo cha amali mkokotoni kaskazini .
Amesema kumekuwa na taarifa nyingi zinazoripotiwa kuwa mkoa huo unatahadharishwa amani ya wananchi na wageni wanaoingia nchini kuwafanyia vitendo viovu vya uhalifu jambo ambalo linaweza kukosesha mapato ya taifa hasa ukizingatia utalii ndio zao kuu badala ya karafuu huongeza asilimia kubwa kwa nchi hii.
Hivyo amesema kuwa jeshi la ulizi na usala wanawajibu wa kuwashughulikia watu ambao wanaokwenda kinyume na sheria za nchi bila umuonea mtu haya.
Aidha amewataka askari jamii kuacha kuacha kuchukua sheria mikononi mwao na wafuate utaratibu uliowekwa na nchi na washirikiane na wananchi ili kuleta maendeleo,
pia waziri mohamed aboud amesema hivi sasa kumekua na tatizo la kuongezeka kero za ajali barabarani hivyo jeshi la police linajukumu la kuzuiya ajali hizo na kupunguza vifo vinavyotokana na ajali hizo
nao masheha walitoa michango yao mbali mbali yanayowakumba katika kazi zao na kutaka waziri kuzifanyia zazi changamoto hizo.