VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WAMETAKIWA KUWA WAADILIFU

 

Viongozi  wa  vyama  vya  ushirika  wametakiwa  kuwa  waadilifu katika  kutunza  mali  za  vikundi  hivyo  ili  kujenga  imani  kwa  wanachama  kwamba  kujiunga  kwao  kuna  manufaa.

Mrajis  wa  vyama  vya  ushirika  zanzibar, khamis  daudi  simba, amesema  kuwa  baadhi   viongozi   wamekuwa  wakijisahau  kutimiza  wajibu  wao  pindi  wanapopewa  dhamana  za  uongozi  na  kusababisha  wanachama  kuvunjika  moyo  kuendelea  katika  vikundi  vyao  na  kurudisha  nyuma  matarajio  ya  wengi  ya  kujikomboa  kimaisha.

Akizungumza  katika  mkutano  wa  uchaguzi  wa  muungano  wa  vyama  vya  ushirika  zanzibar  cuza, amewakumbusha  viongozi  watakaopewa  dhamana  kuzingatia  katiba za  vyama  zinavyoelekeza  kwa  kufanya  vikao  kila  mwaka  kutahmini  mwenendo  wa  shughuli  zao.

Kwa  upande  wake  kaimu  katibu  mtendaji  wa  cuza, nd. Suleiman  mbarouk, amesema  wanatarajia  kujiimarisha  zaidi  katika  kilimo  endapo  serikali  uitawaongezea  nguvu  waweze  kuendesha  shughuli  zao  kwa  ufanisi.

Mapema  naibu  waziri  wizara  ya  kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake  na  watoto, mh.  Shadya muhamed  suleiman  amewakumbusha  viongozi  hao  kujipanga upya  na  kujitathmini  ili  kuepuka  kasoro  zilizojitokeza  hapo  kabla.