VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WAWE WABUNIFU

 

Viongozi wa vyama vya ushirika wametakiwa  wawe wabunifu zaidi katika kuongeza kipato na faida ya ushirika wao.

Akizungumza katika  mkutano wa 17 ushirika wa elimu Saccos  mwenyekiti wa ushirika wa akiba na mikopo elimu nd Ahmed Omar amesema vikundi vingi vya ushirika vimekuwa vikiyumba kutokana na viongozi wao kushindwa kuwa wabunifu wa kuongeza mitaji.

Aidha amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kuwa waadilifu katika kutunza mali za ushirika pamoja na kuwa karibu na wanachama wao ili kuwaridhisha.

Nao baadhi ya wanachama wa elimu saccos wameelezea mafanikio yaliyopatika  na kuwashauri watu wengine kujiunga na ushirika wao ili kufaidika na fursa zinazopatikana katika ushirika wao ikiwemo mikopo ya fedha na vifaa.