VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUTOKUWA VIKWAZO KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUMU YAO

Katibu mkuu wa shirikisho wa vyama vya wafanyakazi zanzibar (zatuc) nd. Khamis mwinyi mohamed, amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutokuwa vikwazo katika utekelezaji wa majumu ya ili waweze kusimamia na kutetea maslahi ya wafanyakazi.
Akifungua mkutano wa nne wa mpango kazi wa mwaka 2018 wa baraza kuu la chama cha wafanyakazi wa huduma za umma zanzibar [zapswu] katika chuo cha utalii maruhubi, nd khamis amesema vyama hivyo vipo kwa ajili ya kuwaunganisha wanachama na kutatua migogoro inayojitokeza katika sehemu zao za kazi,hivyo kuwepo kwa vikwazo hakutosaidia katika kufikia lengo lililo kusudiwa
Nae naibu katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi serikali za mitaa tanzania [talgwu] nd. Obadia mwakasitu amewataka wanachama kutambua wajibu na majukumu yao ya kazi baada ya kupata ajira ili kuepusha matatizo katika kazi zao.
Akizungumzia juu ya mkutano huo, mwenyekiti wa taifa wa chama cha wafanyakazi wa huduma za umma zanzibar, nd. Ameir mwadini nahoda, amesema kikao hicho cha siku mbili kitapitisha marekebisho ya kanuni za utumishi na kanuni ya fedha ili kutolewa maamuzi na baraza kuu