VIONGOZI WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA (AU) WANAKUTANA JIJINI ADDIS ABABA

Viongozi wakuu wa nchi na serikali wa umoja wa Afrika (AU) wanakutana jijini Addis Ababa- Ethiopia utakaojadili masuala mbalimbali ya umoja huo ya kuimarisha ulinzi na usalama na maendeleo ya kiuchumi Barani Afrika.

miongoni mwa masuala hayo ni pamoja na hali ya ulinzi na usalama katika bara la Afrika hasa kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- Drc na Libya.

aidha viongozi hao watajadili hali ya usalama katika baadhi ya nchi zilizoathiriwa na kundi la boko haram na uanzishwaji eneo huru la kibiashara kwa ajili ya kukuza biashara kwa nchi wanachama pamoja na kupunguza utegemezi kwa masoko ya nje barani afrika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo akimwakilishwa na Rais John Pombe Magufuli.

kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni kuimarisha mgawanyiko wa idadi ya watu kupitia uwekezaji katika vijana.