VIONGOZI WAMESISITIZWA KUWA MAKINI KATIKA KUSIMAMIA MAJUKUMU YAO

Viongozi wa chama cha mappinduzi wamesisitizwa kuwa makini na kusimamia ipasavyo uchaguzi wa chama na jumuiya zake unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Wawakilishi wa viti maalum mkoa wa kaskazini unguja MH. Riziki Pembe Juma na MH. Panya Ali Abdalla wakizungumza na makatibu wa matawi wa mkoa huo wamesema kufanya hivyo kutaondoa malalamiko yanayojitokeza katika uchaguzi kwa baadhi ya washiriki wanaogombania nafasi za uongozi.
Wakizungumzia malengo ya chama katika kujikwamua na umasikini wamewataka viongozi hao kukaa pamoja na kubuni miradi ambayo itawasaidia katika jumuiya zao na kufikia malengo.
Baadhi ya makatibu wa jumuiya ya uwt wameahidi kutekeleza kwa umakini majukumu yao na kuhakikisha chama kinafikia malengo yake.
Wakati huo huo mh. Riziki alisimama kwa muda, baada ya kuwaona wanafunzi wa skuli ya chaani wakizurura nje ya maeneo ya skuli wakati wa masomo na kukutana na viongozi wa skuli hiyo ili kujua utaratibu wa ufundishaji katika skuli hiyo.