VIONGOZI WAMETAKIWA KUIELIMISHA JAMII JUU ATHARI YA VITENDO VYA WIZI WA MAZAO NA MIFUGO

Mwenyekiti wa bodi ya mtandao mkoa kaskazini unguja ali omar makame, amsema vitendo vya wizi wa mifugo na mazao vinavyofanywa na baadhi ya vijana vimekuwa vikirudisha nyuma jitihada za wananchi za kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na viongozi wa mabaraza ya vijana, masheha, madiwani na makundi yenye mahitaji maalum wa mkoa kaskazini unguja, amesema vitendo vya wizi vinachangiwa zaidi na kuporomoka kwa maadili, hivyo amewataka viongozi hao kuielimisha jamii juu athari ya vitendo hivyo.
Amesema kumekuwa na kisingizio kinachodaiwa kuchangia kutokea kwa vitendo hivyo, ikiwemo ukosefu wa ajira, jambo ambalo amesema halina ukweli kwani mkoa huo umekuwa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi.
Wakichangia viongozi hao wamependekeza kufikishiwa elimu vijana katika maeneo yao ili kuachana na vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili, ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya ambayo ni chanzo kikuku cha kutokea vitendo vya wizi.
Afisa mradi wa ushirikishwaji vijana katika sera za kitaifa mkoa kaskazini unguja, nd khamis hassan kheri, amesema wamekuwa na mkakati wa kuwajengea uwezo vijana kuweza kujitambua na kuweza kuwaelimisha wengine.
Mafunzo hayo yameansdaliwa na matandao wa asasi za kiraia mkoa kaskazini unguja kwa ufadhili wa the foundation for civil soceyt ya dares salaam