VITA KATI YA IRAQ NA WAPIGANAJI WA ISLAMIC STATE VIKIENDELEA KUSHIKA KASI

Huku vita kati ya serikali ya iraq na wapiganaji wa islamic state vikiendelea kushika kasi mjini mosul, raia waliokwama katika mji huo watakabiliwa na majanga makubwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka umoja wa mataifa.
mratibu wa misaada ya kibinadam wa umoja huo, amesema , raia wa mosul wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, maji, dawa na umeme.
Kumeibuka ripoti kwamba walenga shabaha wa islamic state wamekuwa wakiwauwa watoto kwa makusudi nchini humo. .
Wanajeshi wanasema kuwa wamepiga hatua kwa saa chache wanapojaribu kuwatimua wanamgambo hao kutoka ngome zao za mwisho katika mji wa zamani wa mosul.
Maelf ya raia wameukimbia mji huo wa kaskazini tangu jitihada za kuukomboa zianze tangu oktoba mwaka uliopita.