VITENDO VYA UKATILI BADO VINAENDELEA ZANZIBAR

Vitendo vya ukatili bado vinaendelea zanzibar mtu mmoja alietambulika kwa jina la kauthar ashrak mkaazi wa kisima mbaazi amejeruhiwa vibaya baada ya kuunguzwa moto uliomsababishia kupata maumivu makali mwlinii mwake na kulazimika kusafirishwa kwenda dar es salam kwa ajili ya kupata matibabu zaidi
Akisimulia mkasa huo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa zanzibar majeruhi huyo amesema majira ya saa 12 za asubuhi wakati akiwataarisha wanawe kwa ajili ya kwenda skuli alikwenda mtu nyumbani kwake na kugonga mlango,baada ya kumfungulia alimwagia mafuta ya taa na kumu washa moto kwa kutumia kibiriti jambo ambalo limemsababishia maumivu makali
mama mdogo wa majeruhi huyo msim mwalim amedai kuwa tukio hilo huenda limesababishwa na kukosekana kwa maelewano kati ya kauthar na mpangaji wake ameiyomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya watu wanaotenda vitendo vya ukatili
Mkuu wa kitengo cha dharura cha hospitali ya al rahma doctor fahad nassor amesema wamempokea mgonjwa huyo majira ya saa 12 na nusu asubuhi na kumpatia huduma ya dharura kabla ya kusafirishwa kwenda hospitali ya muhimbili ya dar es salaam